tiko
tiko
Daktari bingwa wa zamani wa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Dk Fulgence Mosha
Daktari
bingwa wa zamani wa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Dk
Fulgence Mosha anasotea mafao yake ya kiinua mgongo na pensheni kwa
miaka 10 mfululizo bila mafanikio.
Akizungumza juzi, Dk Mosha alisema licha
ya kulifikisha suala hilo kwenye vyombo husika, ikiwamo Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora, bado mafao yake ni kitendawili.
Dk Mosha aliajiriwa na Serikali mwaka
1983 kabla ya Januari 1,1995 kupelekwa KCMC kwa barua ya Desemba 29,
1994 yenye kumb HE/MP ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Desemba 11, 2004, Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii ikauandikia barua uongozi wa KCMC kutoa kibali cha Dk
Mosha kustaafu rasmi baada ya kufikisha umri wa miaka 60 wa kustaafu
kisheria.
Alisema baada ya kustaafu, alilipwa Sh10
milioni na Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF), ikiwa ni michango yake
na ya mwajiri ambaye ni Shirika la Msamaria Mwema (GSF) linalomiliki
KCMC.
“Katika utumishi wangu nimefanya
operesheni kubwa zaidi ya 7,000 zikiwamo za viongozi wakuu wa nchi hii
lakini leo baada ya kustaafu napigwa danadana sina thamani tena kwa
Serikali,” alisema.
Kwa mujibu wa Dk Mosha, utata wa mafao
yake ikiwamo kulipwa pensheni kila mwezi, unatokana na Hazina kutopeleka
mchango wowote katika Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).
Dk Mosha alisema baada ya kustaafu,
alichukua malipo yake ya NSSF na kuyapeleka PSPF ili yajumlishwe na
michango ya Serikali katika kipindi alichokuwa mtumishi wa Umma
(1983-1994).
“Zile fedha zilikaa kule, PSPF wakaamua
kunirudishia maana Serikali haikupeleka ile michango yake ambayo
walitakiwa wailipe kati ya 1983 na 1994 nilipokuwa serikalini,” alisema.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia
Kabaka, alipoulizwa na gazeti hili kuhusu malalamiko ya Dk Mosha
alionyesha kushtushwa na kusema, huenda daktari huyo hakutumia njia
sahihi kudai haki yake.
“Simfahamu huyo daktari lakini ni jambo
linaloshtua. Naomba mwelekeze aje ofisini na nyaraka zake zote nimpeleke
SSRA (Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii),” alisema
Kabaka.
Kwa mujibu wa Kabaka, kwa sasa zipo
kanuni zinazounganisha mafao kama mfanyakazi alifanya kazi katika maeneo
mawili yanayohudumiwa na mifuko miwili tofauti ya hifadhi ya jamii
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment