tiko
tiko
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu
ASKARI mmoja wa wanyama pori na msaidizi wake wameuawa kwa kupigwa mawe, mapanga, marungu na nondo na wananchi katika kijiji cha Namonge Wilayani Bukombe Mkoani Geita wakituhumiwa kuwa majambazi.
ASKARI mmoja wa wanyama pori na msaidizi wake wameuawa kwa kupigwa mawe, mapanga, marungu na nondo na wananchi katika kijiji cha Namonge Wilayani Bukombe Mkoani Geita wakituhumiwa kuwa majambazi na tayari watu 24 wanashikiliwa akiwemo Afisa mtendaji wa kijiji hicho.
Tukio
hilo limetokea jana jioni baada ya wananchi hao kuhamasishana
wakakusanyika na kuivunja ofisi ya Serikali ya kijiji hicho walimokuwa
wamehifadhiwa kwa usalama wao na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Andrea
Malise wakati akifanya jitihada za kuwasiliana na Polisi ili wafike eneo
la tukio kuwaokoa watu hao bila ya mafanikio.
Akithibitisha
leo asubuhi kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Bukombe Amani
Mwenegoha amesema watu 24 akiwemo Afisa mtendaji wa kijiji hicho
wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi mkali unaendelea.
''Ni
kweli Askari na msaidizi wake wa wanyama pori wameuawa na majina yao
yatapatikana baadaye wameuawa katika mazingira yanayodaiwa na tayari
kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya kitakutana dharura leo
mchana kujadili tukio hilo ..kwani vitendo vya aina hii haviwezi
kuvumiliwa vya kujichukulia sheria mikononi''alisisitiza Mwenegoha.
Wakisimulia
chanzo cha tukio hilo kijijini hapo baadhi ya wananchi wamedai
waliwaona jana alasiri watu watano mmoja wao akiwa na silaha aina ya SMG
lakini baadaye waliwaona wakipita na baada ya muda kupita waliouawa
walirudi na kuingia Bar wakiwa na pikipiki lakini bila silaha kutokana
na kuonekana wageni ndipo wanakijiji walianza kuhoji na kuwasiliana juu
ya watu hao.
Pasipo
subira inadaiwa wananchi walianza kuwatupia mawe na ndipo Afisa
mtendaji wakijiji hicho Alipoingilia kati na kuwaweka katia ofisis yake
kukwepa vipigo kutoka kwa wananchi huku akiwalsaina na polisi wa kituo
cha Lunzewe kilichopo umbali kama kilometa 30 ambapo wananchi walianza
kushambulia jengo la ofisi na kulivunja milango na madirisha.
Baada
ya kufanikiwa kulivunja jengo la ofisi ya serikali ya kijiji waliweza
kuwashambulia watu hao hadi kuwaua na kisha kuchukua kila kitu
walichokuwa nacho ikiwemo fedha walizokuwa nazo mfukoni na kuiharibu
pikipiki waliyokuwa nayo wakigawana vifaa vyake zikiwemo tairi na taa na
kuacha frame peke yake kabla ya Askari polisi kufika eneo la tukio na
kutawanyika.
Chanzo
cha mkasa huo kinadaiwa Askari hao wawili waki wamevaa kiraia wakiwa na
pikipiki baada ya kurudi tena wakiwa bila ya wenzao waliokuwa na
Bunduki waliingia Baa na kuanza kupata kinywaji na ndipo wananchi
walipoanza kuwasiliana kuhoji juu yao na kisha kuhamasishana
kuwashambulia kwa madai huenda walikuwa ni majambazi.
Habari
zaidi kutoka eneo la tukio na kuthibitshwa na Afisa mtendaji wa kata ya
Namonge Charles John amesema Askari hao waliuawa baada ya ofisi ya
serikali ya kijiji kuvunjwa na wananchi na kisha kuanza kuwashambulia
watu hao wakidai kuwa ni majambazi kabla ya kutambuliwa na Askari
wanyama pori waliofika eneo la tukio na kudai walikuwa ni Askari wa
wanyamapori wenzao.
''Askari
hao kufika kijijini ..bila kuripoti ofisi ya kijiji wala Kata kunaweza
kuwa kumechangia kwa kiasi kikubwa kutokea mkasa huo kutokana na ukweli
uongozi wakijiji na kata haukuwa na taarifa ya kuwepo na ujio wa Askari
hao hivyo kushindwa kuchukua hatua mapema hii ni hatari sana kuingia
katika kijiji bila taarifa kinyemela'' alidai John.
Hofu
ya wananchi inadaiwa kuchangiwa na kuwepo kwa matukio ya uhalifu mara
kwa mara katika ukanda huo likiwemo la mnada wa ng'ombe kuvamiwa na watu
wenye silaha Januari 16 na Watu wengine wenye silaha kuingia katika
kijiji cha Ilyamchele Januari 19 na kuwateka wanakijiji baada ya
kuwakirimu.
Pamoja
na kuwepo mazingira na utetezi huo imedaiwa kuwa serikali isipochukua
hatua kali kukomesha vitendo vya ubebaji sheria mikononi kuna hatari ya
kuibuka tabia ya kulipizana kisasi na kubambikiziana tuhuma na hivyo
kukosekana kwa utawala wa sheria na kikatiba na kuuawa wasio na hatia.
Kufuatia
tukio hilo mamia ya wanaume wanadaiwa kukimbia kaya zao na kutokomea
kusikojulikana kutokana na kuhofia kukamatwa na hivyo familia kubakiwa
na wanawake, vikongwe na walemavu pake yao.
tiko
tiko
Post a Comment