tiko
tiko
Ama kwa hakika leo haikuwa siku nzuri kwa vijana wa Jose Mourinho – klabu ya Chelsea.
Wakicheza dhidi ya moja ya timu zinazopigania kutoshuka daraja – Burnley, Chelsea leo imempoteza mchezaji wake muhimu Nemanja Matic ambaye amefungiwa mechi 3 kutokana na kupata kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Wakiwa kwenyee uwanja wao wa nyumbani – Stamford Bridge, Chelsea walipunguzwa kasi baada ta kutoka sare ya 1-1 na Burnley.
Chelsea walianza kupata goli mapema katika dakika ya 16 ya mchezo huo mfungaji akiwa Branslav Ivanovic, lakini huku baadhi ya mashabiki wakijua leo Chelsea wangetoka na ushindi – Burnley wakasawazisha kupitia goli la Ben Mee katika dakika za mwisho za mchezo huo.
Kwa matokeo hayo Chelsea wanaendelea kushika usukani mwa EPL huku wakifukuziwa na City.
tiko
tiko
Post a Comment