tiko
tiko
Wakiwa na mfululizo mzuri wa matokeo ya ndani ya uwanja – vijana wa Arsene Wenger leo walikuwa wanakutana na Crystal Palace katika mechi za raundi ya pili ya ligi kuu ya England.
Mchezo uliopigwa katika dimba la Selhurst Park umeshuhudia Arsenal wakipanda mpaka nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kwa kuwafunga Palace kwa magoli 2-1.
Arsenal walianza kupata goli katika kipindi cha kwanza kupitia mkwaju wa penati wa Santi Cazorla.
Kipindi cha pili Olivier Giroud aliongeza goli la pili baada ya pasi nzuri kutoka kwa Danny Welbeck, lakini dakika za majeruhi Crystal Palace walilisakama lango la Arsenal na Murray alifanikiwa kufunga goli la kufutia machozi.
tiko
tiko
Post a Comment