tiko
tiko
Dully akilia kwa simanzi wakati akipewa pole na waombolezaji waliofika msibani Mbezi Beach, Dar leo mchana.
MAZISHI ya mwanamuziki mkongwe nchini ambaye ni baba mzazi wa
mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, Ebby Sykes yatafanyika leo saa
10 jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mzee Sykes alifariki dunia jana mchana akiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa
vidonda miguuni vilivyopelekea kueneza sumu katika mwili wake na
kumsababishia mauti.
Kwa mujibu wa Dully, Mzee Sykes alikuwa akisumbuliwa na vidonda hivyo
vilivyoshindwa kupona kutokana na kuvuta sigara. Lakini mbali na hilo
hakuwa na tatizo lingine lolote.
Mzee Sykes amefariki akiwa na umri wa miaka 62 alizaliwa Februari 24, 1952.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment