tiko
tiko
Shule za sekondari za Serikali zinazochukua watoto wenye vipaji, zimeshindwa kung'aa kwenye matokeo ya kidato cha nne 2014 huku shule ya Ilboru ya mjini Arusha ikiwa ni shule ya kwanza ya Serikali na iko nafasi ya 35 kati ya shule 2,320 zilizofanya mtihani wa kidato cha nne 2014.
Mwaka
2013, Ilboru ilishika nafasi ya 41 chini ya shule nyingine yenye vipaji
ya Mzumbe ambayo katika matokeo ya sasa imeshika nafasi ya 56 na
kushika nafasi ya pili katika shule za Serikali.
Wanafunzi
94 wa Ilboru walijisajili kwa ajili ya mtihani huo, huku watahiniwa 90
wakifaulu (distinction, merit, credit na pass) na wanafunzi watatu
wakifeli. Ilboru ina wastani wa pointi GPA 3.74.
Mzumbe
iliyoporomoka kwa nafasi 16 ukilinganisha na mwaka 2013, wanafunzi
watahiniwa 110 wamefaulu na mmoja akifeli na ina GPA 3.47.
Msalato
ambayo mwaka 2013 ilishika nafasi ya 63, imeshika nafasi 71 ikiwa na
GPA 3.30 huku watahiniwa 85 wamefaulu. Mwaka 2013 shule hiyo ilishika
nafasi ya 65.
Kibaha
ikiwa miongoni mwa shule za vipaji imeporomoka nafasi 43, ikishika
nafasi ya 87 baada ya kupata GPA 3.22, ambapo watahiniwa 98 wakifaulu na
wanne kufeli. Mwaka 2013, shule hiyo ilikuwa nafasi ya 44.
Shule
ya wavulana ya Tabora imeporomoka kwa nafasi 37 ukilinganisha na
matokeo ya mwaka 2013. Shule hiyo imeshika nafasi ya 93 ikiwa na GPA
3.18 ambapo wanafunzi 96 wakifaulu na wanne wakifeli. Mwaka 2013 ilikuwa
nafasi ya 56.
Kilakala
ambayo mwaka jana ilikuwa nafasi ya 63, imeshuka hadi nafasi ya 96
ikiwa na GPA ya 3.13, huku wanafunzi 80 wakifaulu na wanafunzi watatu
wakifeli mtihani huo.
Katika
kundi la shule zenye vipaji, shule ya wasichana ya Tabora ambayo
matokeo yaliyopita (2013) ilishika nafasi ya 147 zimezidi kuporomoka na
kushika nafasi ya 295 ikiwa na GPA ya 2.24. Wanafunzi 57 wamefaulu na
watano wakifeli.
Kwa
upande wa shule kongwe za jijini Dar es Salaam Jangwani imeporomoka
kutoka nafasi ya 226 mwaka 2013 hadi kufikia nafasi ya 243 ikiwa na GPA
2.42, Azania iko nafasi ya 427, Zanaki (270), Bwiru (234) na Pugu (420).
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment