tiko
tiko
STAA wa
filamu za Kibongo, Wema Sepetu amemfanyia ‘sapraizi’ msanii mkongwe,
Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ kwa kumnunulia simu ya kisasa na kumfanya
awe kama kijana.

Staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.
Wema alimfanyia sapraizi hiyo hivi karibuni kwa kummpeleka Bi.Mwenda
katika maduka ya Mlimani City pasipo kumwambia wanakwenda kufanya nini
na alipofika, akamnunulia simu hiyo yenye uwezo wa ‘internet’.
Msanii mkongwe, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’.
“Namshukuru sana Wema maana sikujua tunakwenda kufanya nini Mlimani
City, nikashangaa ananikabidhi simu, nimefurahi na mimi kuwa kama vijana
wa kisasa, kuingia WhatsApp na Instagram,” alisema Bi. Mwenda.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment