tiko
tiko
Hali si shwari hata kidogo! Wikiendi iliyopita staa wa sinema za
Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ alijikuta akiangua kilio na kuungwa mkono na
mastaa wenzake, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ na Single Mtambalike
‘Richie’ walipomtembelea wodini mama mzazi wa mtoto Albino, Yohana
Bahati (1) aliyeuawa kikatili, Ester Thomas (30) ambaye naye alijeruhiwa
vibaya kichwani, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha.
Staa
wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ akiwa na Amri Athumani ‘Mzee
Majuto’walipomtembelea wodini mama mzazi wa mtoto Albino, Yohana Bahati
(1) aliyeuawa kikatili, Ester Thomas.
Tukio hilo la majonzi lilijiri kwenye Hospitali ya Bugando mkoani hapa
ambapo wasanii hao walikwenda kumfariji mama wa mtoto huyo aliyetekwa
mjini Geita hivi karibuni.
Walipofika wodini hapo, JB na wenzake walitoa yao ya moyoni kupinga
vikali ukatili aliotendewa mama huyo na mwanaye huku wakitahadharisha
juu ya laana inayoweza kuikumba jamii yetu kwa tukio hilo.
JB: Nampa pole sana mama Yohana. Hii ni aibu kubwa kwa taifa letu na jamii pana duniani.
Watu hawafanyi kazi kujipatia kipato halali. Mafisadi wanataka kujipatia fedha kupitia njia za kishetani za kuwaua wenzetu. Albino ni wenzetu na tunawapenda. Lazima wahalifu wakamatwe na wahukumiwe kunyongwa.

Mzee Majuto: Inasikitisha sana. Haivumiliki. Albino ni wenzetu na wana
uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa letu. Wahusila lazima wakamatwe na
tuone wakichukuliwa hatua kali.
Richie: Natokwa na machozi. Hiki ni nini? Hatuwezi kufumbia macho jambo hili hasa sisi wenye nafasi kubwa ya kukemea vitendo hivi.
Richie: Natokwa na machozi. Hiki ni nini? Hatuwezi kufumbia macho jambo hili hasa sisi wenye nafasi kubwa ya kukemea vitendo hivi.
Mara baada ya mastaa hao kutoa la moyoni katika wodi aliyolazwa mama
huyo, iligeuka kama msiba kwani kila aliyekuwepo alikuwa akiangua kilio
kwa uchungu.
Tayari mtoto Bahati amezikwa baada ya mwili wake kupatikana ukiwa hauna
baadhi ya viungo huku mama yake akiendelea na matibabu baada ya
kufanyiwa oparesheni sehemu ya kichwani aliyojeruhiwa vibaya wakati
akinyang’anywa mwanaye.
KUTOKA KWA MHARIRI
Global Publishers tunaungana na dunia nzima kukemea vikali mauaji ya Albino ambayo rekodi inaonesha hutokea wakati wa uchaguzi mkuu hivyo tunavitaka vyombo husika kufanya kazi yake ili kuliondolea taifa aibu hii nzito.

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment