tiko
tiko
Alikuwa wapi? Baada ya kupotea kwa muda mrefu, staa wa sinema na muziki
wa Bongo Fleva, Snura Mushi hatimaye ameibuka na kueleza sababu za
ukimya wake.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum, Snura amefunguka
kwamba ukimya wake ulitokana na kwenda Afrika Kusini ‘Sauz’ kushuti
video ya wimbo wake wa Najidabua na siyo kweli kwamba alikuwa mkoani
Mbeya kwa mwanaume.
Katika intavyu hiyo, Snura alikanusha tetesi za kuzaa mtoto wa pili na
kusisitiza ana mtoto mmoja na wanaosema maneno hayo wamekosa la
kusema.Ijumaa Wikienda: Huoni kukaa kwako kimya mashabiki
wamekusahau?Snura: Hawajanisahau kabisa na hilo nililithibitisha hivi
karibuni kwenye shoo niliyofanya Msasani Club (Dar), ambapo walijaa
tofauti na mwanzo japokuwa mwanzoni kabla ya shoo nilikuwa nawaza
wamenisahau.
Walifurahi sana kwani kwa sasa nimekuja na staili tofauti ya kukata
mauno ambayo inatambulika kwa jina la Mauno ya Panya Road, yaani haya ni
hatari.Ijumaa Wikienda: Kuna habari kwamba wewe na mpenzi wako DJ
Hunter wa Mbeya mmeachana, hili likoje?
Snura: Unajua katika maisha yangu Hunter ndiye mwanaume wa kwanza
kumuanika na sikuwahi kuanika mapenzi yangu kabisa kabla ya hapo. Sasa
baada ya kuwa tunatupia picha mbalimbali kwenye mitandao watu
walinifuata na kunieleza kwamba ninavyofanya siyo vizuri.
Nilichukua ushauri wao na kuufanyia kazi na mpenzi wangu nikamwambia, tukaacha tabia hiyo.
Hali hiyo ya kutokuweka picha ndiyo iliyozusha maneno kibao kwamba tumeachana lakini siyo kweli.
Ijumaa Wikienda: Hivi huoni kwamba Shilole amekufunika kwa sasa wakati wewe ulikuwa juu zaidi yake?
Snura: Hicho kitu hakipo na Shilole hawezi kunifunika kwani najua kwamba siku zote mbuyu hauwezi kugeuka mchicha.
Hali hiyo ya kutokuweka picha ndiyo iliyozusha maneno kibao kwamba tumeachana lakini siyo kweli.
Ijumaa Wikienda: Hivi huoni kwamba Shilole amekufunika kwa sasa wakati wewe ulikuwa juu zaidi yake?
Snura: Hicho kitu hakipo na Shilole hawezi kunifunika kwani najua kwamba siku zote mbuyu hauwezi kugeuka mchicha.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment