tiko
tiko
Jeshi la
wananchi kwa kushirikiana na polisi nchini limeongeza askari wa vikosi
vya ardhini katika zoezi la kukabiliana na vikundi vinavyodaiwa kuwa vya
kigaidi katika mapango ya mleni yaliyopo eneo la amboni jijini Tanga
kufuatia askari wa jeshi la wananchi kuuawa kwa risasi huku wengine
wakijeruhiwa katika mapigano baina yao na vikundi hivyo.
Paparazi
imeshuhudia msafara wa magari ya kijeshi pamoja na yale ya maofisa wa
kijeshi na huduma ya kwanza yakipita katika barabara kuu itokayo Tanga
kwenda Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania kisha kuingia katika njia
iendayo katika mapango yaliyodaiwa kuwa ni sehemu maalum ya maficho ya
vikundi hivyo vya kigaidi na msemaji wa polisi kamishna wa polisi
-operesheni Paul Chagonja kutwa nzima simu yake iliita bila majibu
lakini msaidizi wake alipoke na kudai kuwa bosi wake yupo kwenye kikao.
Hata hivyo
baadhi ya familia zilizopo katika eneo la mleni zinadaiwa kuhamisha
makazi kufuatia milipuko ya risasi na silaha nzito za kijeshi zilizokuwa
zikirindima katika kipindi cha siku mbili nyakati za mchana na usiku
hatua ambayo baadhi ya makundi ya vijana yanaojihusisha na kazi ya
kupasua mawe katika mapango hayo kulalamikia ukosefu wa kazi kwa sababu
ya mapigano hayo ambayo pia yamewapa hofu na maisha yao.
Baadhi ya wakazi
wa jiji la Tanga wameshauri mapango hayo yaharibiwe kwa kutumia vifaa
maalum vya kivita na jeshi la polisi lisahau suala la silaha zao
zilizoibwa katika matukio tofauti na makundi hayo.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment