tiko
tiko
WAJAWAZITO
katika Kijiji cha Msisi wilayani Bahi, mkoani Dodoma wanajifungulia
sakafuni kwenye jengo la wazi, hali inayosababisha kukosa faragha.
Kutokana
na kadhia hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Betty Mkwasa ameahidi kutoa Sh
500,000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi za chumba cha kujifungulia
akinamama hao.
Hayo
yalibainishwa hivi karibuni wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa
Wilaya ya Bahi, ambapo Diwani wa viti maalumu Kata ya Msisi, Dominica
Nyau aliomba juhudi za makusudi zichukuliwe ili ujenzi wa wodi ya
kujifungulia akinamama wajawazito ukamilike kutokana na wanawake hao
kujifungulia sakafuni.
Alisema mwanamke anapojifungulia sakafuni hata usalama wa mtoto unakuwa ni mdogo kulingana na mazingira yake.
Alisema
wanawake wanaofika kwa ajili ya kujifungua kwenye zahanati hiyo,
wamekuwa wakijifungulia mahali ambapo hapana usiri kutokana kuuwepo na
chumba ambacho hakimsitiri mwanamke kwa ajili ya shughuli hiyo.
Kwa
mujibu wa diwani wa kata hiyo, Novemba Mosi, mwaka 2012, jengo la wodi
ya kujifungulia katika zahanati ya kijiji hicho liliezuliwa na mvua
iliyoambatana na upepo mkali, na kufanya akinamama kukosa mahali pa
kujifungulia kutokana na ukarabati wake kuchukua muda mrefu.
Alisema
juhudi mbalimbali zilifanyika ikiwamo kufikisha taarifa kwenye Baraza
la Madiwani kupitia kamati za kudumu za afya, elimu na maji, ili
halmashauri ifanye tathimini ambapo halmashauri iliomba Tamisemi kama
maombi maalumu ili jengo hilo lifanyiwe ukarabati lakini ombi lao
halikukubaliwa.
Licha
ya kuomba juhudi kuchukuliwa kukamilisha ujenzi huo Mkwasa aliahidi
kutoa Sh 500,000 na mifuko kadhaa ya saruji, ili kuhakikisa ujenzi huo
wa wodi ya kinamama kujifungulia unakamilika.
Alisema akiwa kama mwanamke ameguswa na tatizo hilo kwani kujifungulia sakafuni wakati wa uchungu ni adhabu kubwa kwa akinamama.
tiko
tiko

Post a Comment