tiko
tiko
WAKATI wagonjwa
wakifa kwa kukosa dawa hata kidonge kimoja kwenye hospitali mbalimbali
nchini, katika hali ya kushangaza, shehena kubwa ya madawa katika
Hospitali Rufaa ya Morogoro imeteketezwa kwa moto baada ya kuharibika
kwa kupita muda wake wa matumizi, Ijumaa Wikienda linakuwa la kwanza
kukujuza.
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi
karibuni mjini hapa ambapo paparazi wetu alitonywa kuhusiana na kuwepo
kwa ishu hiyo ambapo alikwenda na kushuhudia lori lenye uzito wa tani 7
likisomba dawa hizo zilizoharibika kwa awamu nne mfululizo na kwenda
kutupa katika dampo lililopo maeneo ya Kihonda-Viwandani.
Kwenye uteketezaji huo, mwanahabari wetu
aliwashuhudia baadhi ya maafisa wa hospitali hiyo waliokuwepo kwenye
dampo hilo wakitaka tukio hilo lirushwe katika vyombo vya habari lakini
wengine wakakataa na kudai libaki kuwa siri.
Ilidaiwa kuwa baadhi ya maofisa waliokuwa wanataka jambo hilo liwe siri, walikuwa wakihofia kunyimwa dawa mpya na Bohari Kuu ya Taifa (MSD).
Ilidaiwa kuwa baadhi ya maofisa waliokuwa wanataka jambo hilo liwe siri, walikuwa wakihofia kunyimwa dawa mpya na Bohari Kuu ya Taifa (MSD).
Mwanahabari wetu alipohoji sababu za
baadhi ya maofisa hao kutaka kulificha tukio hilo, walimjia juu na
kumtaka afute picha za tukio hilo lakini jitihada zao zikagonga mwamba
kwani paparazi wetu alifanikiwa kuwatoka.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
walihoji kulikoni kuwe na shehena kubwa ya madawa yaliyoharibika wakati
wamekuwa wakitaabika wakiambiwa dawa hakuna mara kwa mara wanapokwenda
hospitalini hapo?
Alipotafutwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Mkoa wa Morogoro, Godfrey Mtei na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo,
alikiri kutokea na kudai dawa hizo zilikuwa zimeisha muda wake wa
matumizi na hakukuwa na namna yoyote zaidi ya kuziteketeza kwa moto.
“Ni utaratibu wetu, dawa zikiharibika huwa tunaziteketeza kwa moto,” alisema Mtei.
“Ni utaratibu wetu, dawa zikiharibika huwa tunaziteketeza kwa moto,” alisema Mtei.
tiko
tiko
Post a Comment