tiko
tiko
Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanatarajia kufanya maandamano ya siku tatu mfululizo usiku na mchana jijini Dar es Salaam kuanzia Jumatatu ijayo, kushinikiza kuonana na Rais Jakaya Kikwete kumweleza matatizo ya ajira wanayokabiliana nayo.
Wahitimu
hao jana walifanya mkutano katika eneo la Msimbazi Centre, Dar es
Salaam na Mwenyekiti wa Vijana waliohitimu mafunzo ya JKT, George Mgoba
alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiomba kukutana na Rais ili wamueleze
matatizo wanayokumbana nayo, lakini wamekuwa wakipewa ahadi za uongo na
Katibu Mkuu wa Rais.
“Tumeomba
mara nyingi kukutana na Rais na tumekuwa tukiandika barua, lakini
hatujibiwi chochote. Tunajua hizi ni njama tu za watu wachache wanaozuia
tusionane na Rais,” alidai Mgoba.
Alidai
kuwa wameandika barua nyingine na hivi karibuni Katibu wa Rais
aliwapigia simu kuwa wafike Februari 10 ili waonane na Rais na
walipofika, hawakufanikiwa kumuona Katibu huyo.
Akizungumzia
sababu za kutaka kuonana na Rais, alidai ni kutaka kujua hatma yao ya
kutopatiwa ajira kutokana na mafunzo ya kijeshi waliyoyapata. “Sisi tumepatiwa mafunzo ya kijeshi na sasa tupo uraiani kwa ajili gani? Hawa wote unaowaona ni askari tayari ” alidai.
Mkutano
wao uliwakutanisha pamoja ili kuweka mikakati yao ikiwa ni pamoja na
kufanya maandamano ifikapo Jumatatu kama serikali haijajibu, kama
itawaajiri au hapana. Walidai endapo jibu halitapatikana, basi watafanya
maandamano ya siku tatu mfululizo hadi ombi lao la kumwona Rais
lifanikiwe.
Makamu
Mwenyekiti, Paral Kiwango, alisema jambo hilo linaonekana kuwa na
upendeleo mkubwa, kwani wenzao wa upande wa Zanzibar wote waliomaliza
mafunzo ya JKT, wanapatiwa ajira. Alihoji iweje vijana wa Bara
wametelekezwa?
“Wenzetu
wa upande wa Zanzibar wakimaliza mafunzo wote wanaajiriwa, lakini sisi
Tanzania Bara hakuna anayetujali na kututhamini,” alidai Kiwango.
Kwa
upande wake, Katibu wao Liwus Emmaneul amesema kuna fursa nyingi za
ajira hapa nchini kama vile TANAPA na sehemu zingine, ambazo wao
wanaweza kufanya kazi; lakini wanaoajiriwa kule ni watu wengine
wasiokuwa hata na ujuzi, huku wao wakitelekezwa na wakiomba ajira kule
hawathaminiwi, kama watu wenye maadili na mafunzo.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipotafutwa
ili atoe ufafanuzi juu ya maandamano hayo, simu yake ya mkononi iliita
bila majibu.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment