tiko
tiko

Mwigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu
‘Wema’, amemfungulia kesi ya madai mpenzi wake wa zamani ambaye ni
mwanamuziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, kwa kumtapeli kiasi
cha Sh milioni 10.
Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la
Utangazaji (BBC) idhaa ya Kiswahili, Wema aliripoti madai yake kituo cha
Polisi Oysterbay akidai kuwa alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa
makubaliano ya kazi na kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume
makubaliano yao.
Muhusika mkuu ambaye ni Wema alitoa
maelezo kwamba watu wanamtupia lawama kutokana na hatua aliyofikia,
lakini amedai kuwa amelazimika kufanya hivyo kwa kuwa yeye ndiye
aliyeingia dhamana na taasisi Focus Vicoba kuchukua fedha hizo.
“Naona watu wengi wananilaumu kwa kuwa
nimemfungulia kesi Diamond, pasipo kuelewa kama fedha hizo pia hazikua
zangu bali ni mkopo ambao niliingia dhamana katika taasisi ya utoaji
mikopo ya Vicoba.
“Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema Wema.
“Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema Wema.
Mrembo huyo alieleza muda waliiopeana
ahadi ya kurudisha fedha hizo umepita na Diamond haoneshi dalili ya
kuzirejesha wakati wanatakiwa kuzirudisha kwa wakati .
“Yote haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa kurudisha pesa za watu nimekuwa nikimpigia simu Diamond hataki kupokea simu zangu, lakini kama alitaka kunidhulumu ni bora angejiunga mwenyewe na hawa Vicoba ili apate mkopo na kufanya mambo yake au kama aliona hawezi kwa kujishtukia basi angetumia ile tovuti yao, angepata kwa urahisi na hakuna mtu yeyote angejua kama amekopa ila sio kukimbia kulipa deni la watu,” alisema.
Wema ambae alimwekea dhamana, yupo
katika kipindi kigumu ambacho kinaweza kupelekea kufilisiwa mali zake
ambazo aliziandikisha wakati wa kuchukua mkopo huo ili ziweze kufidia
deni hilo.
Kwa mujibu wa kiongozi wa taasisi hiyo
ambae aligoma kutajwa jina lake gazetini, alisema kuwa ni kweli Wema
alifika katika ofisi zao zilizopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ili
apewe muongozo lakini alipotakiwa kufuata taratibu za kiofisi kama
wanachama wengine wanavyofanya katika vikundi, hakukubaliana na
utaratibu, hivyo kushauriwa ajiunge kupitia tovuti .
Alipotafutwa Meneja wa Wema, Martin
Kadinda, kuzungumzia swala hili alisema hajui chochote kuhusu
kufungulia kwa kesi hiyo, akaomba apewe muda kumtafuta msanii huyo ili
aweze kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, lakini hakueleza nini
kilichojiri na kusisitiza asubiriwe.
Pia alipotafutwa meneja wa Diamond,
Babu Tale, kuzungumzia swala hili alionekana kushtushwa na habari hizo
na kudai kuwa hazina ukweli wowote.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania
tiko
tiko
Post a Comment