tiko
tiko
Msanii mkongwe wa filamu nchini,
Vicent Kigosi a.k.a Ray amejipanga kufanya filamu nyingi za kimataifa
mwaka huu, huku akiweka bayana ataanza na Ghana pamoja na Nigeria.
Kwa mujibu wa tovuti Bongo5 , Ray amesema ndani ya mwaka huu ataweka pembeni kazi za ndani na kujikita kimataifa zaidi.
“Nimepanga kufanya mambo mengi
mwaka huu, lakini mwaka huu movie zangu zote nitafanya International
sitafanya movie yoyote ya hapa hapa kwa sababu kama hapa nishafanya
sana, kwahiyo movie zangu zote nitakazocheza mwaka huu 90% nitacheza
nje, kwahiyo kama kuna lolote ambalo litabadilisha nitawajulisha, ni
mapema sana kusema lakini kitu ambacho ninaweza kuweka wazi ni nitaanza
kazi na Nigeria na Ghana, ndani ya mwezi wa nne nadhani kazi zitakuwa
zimeanza,” alisema Ray.
Mipango hii ya Ray inaonekana kja baada ya mwanadada Wema kwenda Ghana na kufanya filamu na Van Vicker.
tiko
tiko
Post a Comment