Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

WOLPER: BORA NIWE FUNDI NGUO

tiko tiko

Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Wolper’ ameamua kuanika ukweli kuwa sasa hivi anataka kuwa fundi wa kushona nguo ili kuepukana na ‘masnichi’ waliopo kwenye tasnia ya uigizaji.


Akizungumza na  paparazi, Wolper alisema ameamua kujikita huko kwa sababu ameona Bongo Movie hakuna maendeleo zaidi ya umbeya na hata soko la filamu linazidi kushuka.
“Mimi ni msanii wa muda mrefu sana na kwa kazi ambazo tayari nimeshazifanya tangu kipindi hicho mpaka sasa naona tasnia haina maendeleo bali wamejaa masnichi tu yaani umbeyaumbeya tu.” 
“Ni bora niwe fundi nguo ili kuepukana na manenomaneno yanayoendelea na mpaka sasa hivi tayari nimeshaanza kujifunza kushona nguo na nina imani nitakuwa fundi mzuri tu kuliko kutegemea kazi ambayo haina masilahi,” alisema
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top