tiko
tiko
WATU wawili Rugonzibwa Mujunangoma na Theophillo Bwakea wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka ya rushwa baada ya kupokea mgao wa Sh. Milioni 485.1 kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow walizohamishiwa na James Rugemalira.
Swai
alidai kuwa Februari 12, mwaka 2014 mshtakiwa akiwa Injia Mkuu wa REA,
alipokea rushwa ya Sh. Milioni 161.7 kupitia akaunti namba
00410102643901 ya Tegeta Escrow kama zawadi kutoka kwa Mkurugenzi
Rugemalira.
Ilidaiwa
kuwa mshtakiwa alipokea zawadi hiyo baada ya kuwa mjumbe aliyeandaa
sera zinazohusu sekta binafsi kuzalisha na kuuza umeme kwa Tanesco.
Mshtakiwa alikana mashitaka yake.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana na kwamba upelelezi umekamilika.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana na kwamba upelelezi umekamilika.
Hakimu
Moshi alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka serikalini au
wanaofanyakazi katika taasisi zinazotambulika watakaosaini hati ya
dhamana ya Sh. Milioni 20 kila mmoja.
Pia alisema mshtakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam, bila kibali cha mahakama.
Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kesi yake itatajwa Januari 26, mwaka huu.
Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kesi yake itatajwa Januari 26, mwaka huu.
Jana
saa 2:00 asubuhi katika viunga vya mahakama ya Kisutu, watumishi na
watu mbalimbali waliingia katika eneo hilo huku kukiwa na minong’ono
kwamba wanaotuhumiwa ufisadi wa Escrow watafikishwa mahakamani hapo.
Pia
waandishi wa habari waligawanyika katika makundi tofauti huku
wakijadili na kutafatuta wadau wao kujua kuhusu ujio wa watuhumiwa hao.
Mapema jana saa 5:42 asubuhi vigogo hao walitinga mahakamani hapo na kwenda kusomewa mashitaka yao yanayowakabili.
tiko
tiko
Post a Comment