tiko
tiko
Mchezo wa wapenzi kusalitiana umeshamiri
sana kwenye jamii yetu. Ni kitu kinachouma sana lakini cha kushangaza
imefika mahali watu wanaona ni cha kawaida kwa kuwa ni vigumu kumzuia
mtu asikusaliti akiwa ameamua kufanya hivyo.
Kamchezo
haka kapo kwa jinsi zote lakini leo niwazungumzie wasichana ambao
baadhi wamezidisha na kuwaogopesha wanaume wengi kujiingiza kwenye
mapenzi.
Tabia ya msichana kuwa na wapenzi zaidi
ya mmoja hasa kimjinimjini imekuwa ni kama fasheni. Unaweza kusema wewe
uko peke yako kwa huyo uliyenaye lakini kumbe unajidanganya.Hii ni kwa
sababu wengi wanasaliti kwa umakini mkubwa bila ya wanaume kushitukia
huku tamaa ya fedha na vitu vya thamani vikiwa ndiyo chanzo.
Matokeo yake sasa unakuta binti anakuwa na mwanaume wa kumlipia kodi ya nyumba, wa kumfanyia ‘shopping’ na wa kumlisha.
Wenye tabia hiyo wengi wao ni wale
wasichana wazuri ambao wakikatiza mbele za wanaume ni lazima wapate
usumbufu wa hapa na pale. Hawa wanapokosa msimamo wa kusema ‘no’ kwa
wanaume wanaowatokea, matokeo yake ndiyo hayo ya kuwapanga foleni
wanaume.
Kinachoniuma sasa ni kwamba, kuna
wanaume ambao wao wanatafuta wanawake wa kuoa na wanapokutana na
wasichana hawa, hujikuta wakiwekeza ile mbaya wakidhani wamebahatika
kupata wasichana wazuri kumbe wameingia ‘vyoo vya kike’.
Ukitaka kujua ni kwa jinsi gani wanaume
wengi tunasalitiwa na wapenzi wetu, msikilize kijana huyu ambaye ni
mmoja wa waathirika wa tabia hii ya wasichana kujimilikisha wanaume
zaidi ya mmoja.Anasema: “Katika maisha yangu nimekuwa na ndoto za kuwa
na mke mzuri, niliamini nikiwa na kazi nzuri na mke mzuri, maisha yangu
yatakuwa ya furaha sana.
“Mungu akanijaalia nilipomaliza chuo
nikapata kazi na siku moja nikakutana na msichana ambaye hakika alikuwa
chaguo la moyo wangu. Umbo lake lilinivutia sana ila hofu yangu ikawa
kwenye tabia.
“Sikutaka kumkosa, nikajiaminisha kwamba
atakuwa mzuri pia kitabia. Nilipomtokea na kummwagia sera zangu, naye
alionesha kunipenda na hapo ndipo tulipoanzisha uhusiano wetu.
“Siku za mwanzo alionesha kunipenda na
kuniheshimu sana. Sikuona dalili za kusalitiwa licha ya kwamba alipokuwa
mbali na mimi nilihisi mapedeshee wangeweza kuniibia. Uzuri alikuwa
akinipa moyo kwamba, amepita kwa wengi lakini kwangu amefika na wala
nisifikirie kuna siku atanisaliti.
“Siku moja tukiwa chumbani kwangu,
aliumwa ghafla. Hali yake ikawa mbaya, nikawapigia simu ndugu zake na
kuamua kumpeleka hospitalini. Kutokana na kuumwa kule, simu yake ilibidi
nimshikie.“Mara ikaingia simu kutoka kwa mtu aliyeseviwa kwa jina la
Mche Mungu. Sikupokea, ikaita mpaka ikakatika. Baadaye ikaingia sms
iliyoandkwa hivi; Vipi baby, mbona hupokei?”
“Ujumbe
huo ulinishangaza sana, nikagundua kuna mwanaume mwingine anapendwa.
Niliumia sana. Baada ya mchumba wangu kupata nafuu na kumkabidhi simu
yake, alionekana kukosa amani zaidi hasa baada ya kugundua kuwa niliona
sms aliyotumiwa.”
Ushuhuda wa kaka huyu unatupa fundisho
kubwa sana. Wasichana wengi wa mjini ni wazuri na wanayajua mapenzi
kweli lakini wengi wao wametawaliwa na utapeli tena wa kisiri sana.
Unaweza kutokea kumpenda sana lakini
kumbe yeye ana lake jambo, anakuchukulia kama wa kukuchuna tu na nyuma
yako unachagia penzi na wenzako kibao.Kikubwa ni kwamba, unapoingia
kwenye uhusiano na msichana yeyote na ukaona anafaa kuwa mkeo hata kama
utabaini kuwa ni mapepe, fanya haraka umuoe.
Ukishamuoa angalau unaweza kuwa na imani
kwamba hawezi kutoa ‘sukari’ yako kwa mtu mwingine licha ya kwamba,
hata ukimuoa akiamua kukusaliti anaweza.Kinachosaidia ukishamuoa ni
kwamba, atatakiwa kufanya kazi ya ziada sana kukusaliti bila ya wewe
kujua na hata akikusaliti haitakuwa kwa kiwango kikubwa.
Wapo ambao wanaishi mbali na wapenzi
wao, ikifika saa tatu usiku anamuaga mpenzi wake tena kwa maneno matamu
kisha anasema anazima simu. Akishazima simu anakwenda kwenye mishemishe
zake. Wewe uko mbali na unajua mwenzako kalala, kumbe yawezekana kaenda
kwa mwanaume mwingine.
Mimi nadhani ni suala la kuaminiana tu
lakini kiukweli kabisa mke au mume ni rahisi sana kumkontroo lakini
mpenzi tena ambaye mnaishi mbalimbali, ukijiaminisha kwamba hakusaliti,
unajipa moyo tu.
tiko
tiko
Post a Comment