tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha |
JESHI
la polisi mkoani Shinyanga linawasaka walinzi wawili wa kampuni ya
Prosper Security Guard kwa kosa na kuvunja ofisi ya Jambo Oil Mill and
Ginnery Limited kisha kuiba shilingi milioni 1.7 na kutoweka na bunduki
mbili.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari Leo kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Januari 9, mwaka huu saa
moja asubuhi katika mtaa wa Ibadakuli, manispaa ya Shinyanga.
Kamanda
Kamugisha amesema siku hiyo mkurugenzi wa Jambo Ginnery, Mohamed
Hawadhi aligundua ofisi ya kampuni imevunjwa na kuibwa fedha taslimu
shilingi 1.7 zilizokuwa ndani ya kasiki la chuma mali ya kampuni hiyo.
Ameongeza
kuwa katika tukio hilo walinzi wawili wa kampuni ya ulinzi ya Prosper
Security Guard waliokuwa wakilinda ofisi hiyo walitoweka na bunduki
mbili aina ya Shortgun zenye namba F658126 na R65967 pamoja na risasi 7.
Kamanda
Kamugisha amewataja walinzi hao kuwa ni William Ubogo na Eliamani
Simoni ambao bado wanatafutwa na jeshi la polisi ili wakikamatwa hatua
za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment