tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Mkazi
wa kitongoji cha Sofi kijiji cha Mhongolowilayani Kahama Mkoani
Shinyanga, aitwae Juma Ramadhan amenusurika kuuawa na wananchi wa eneo
hilo, kwa madai kuwa wamechoshwa na vitisho na vitendo vya kihalifu
anavyovifanya kwa jamii inayomzunguka.
Akizungumza na DUNIA KIGANJANI ofisini
kwake afisa mtendaji wa mtaa wa Mhongolo Ally Manyama amesema wananchi
kufikia hatua hiyo kumetokana na vituko vya kihalifu ambavyo mtuhumiwa
amekuwa akivifanya ikiwemo kutishia kumuua mke wake.
Tarifa
ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa mtuhumiwa amehamishwa katika eneo
hilo na wananchi hao kwa kuhofiwa kuwa huenda akafanya mauaji ya
kishirikina kwani anahisiwa kuwa ni mchawi.
Manyama
amesema baada ya serikali ya mtaa kuingilia kati suala hilo tayari
wananchi wa eneo la Sofi wamechukua uamuzi wa kumfukuza mtuhumiwa katika
eneo hilo wakihofia kutokewa na vitendo ambavyo vimekuwa vikisemwa na
mtuhumiwa.
Akielezea
tukio hilo mmoja wa wananchi wa eneo hilo John Masalu amesema ni muda
sasa wamekuwa wakipokea taarifa za vitisho toka kwa mtuhumiwa hivyo
wamefikia uamuzi wa kumuhamisha katika eneo hilo.
Kwa
upande wake mtuhumiwa Juma Ramadhan amekana kutoa vitisho vya kumuua
mke wake na kusema haelewi chanzo cha jamii kumshambulia mpaka kumfukuza
katika eneo hilo, na kwamba amekubaliana uamuzi huo wa kuhamishwa.
Hata
hivyo uongozi wa serikali ya mtaa wa Mhongolo kupitia kwa afisa
mtendaji Manyama, umeahidi kulifikisha suala hilo katika vyombo vya dola
wilayani Kahama ili taratibu stahiki ziweze kuchukuliwa.
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment