Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Walijua wanachokunywa ni Whisky, kumbe… Aliyewauzia kafungiwa kufanya biashara.

tiko tiko
Whisky
Jamaa mmoja amefikishwa mahakamani Uingereza, kitendo alichokifanya wengi hawakupendezwa nacho!
Nicholas Stewart alitumia chupa zenye nembo ya Smirnoff, Jack Daniels pamoja na Vodka ili watu wasigundue kwamba anachowauzia haikuwa whisky, chupa hizo zilijazwa mkojo.
Mshtakiwa huyo alikamatwa siku ya pili baada ya kuwauzia wateja kwa wingi mkojo huo aliokuwa amechanganya na maji ambapo alikua akitumia kipimo kile kile ambacho hutumika kupimia whisky.
Whisky III
Mwendesha mashtaka Victoria Cartmell kabla ya kutoa hukumu alipokea majibu kutoka kwa mkemia Mkuu ambapo yalionyesha kwamba kilichokuwa kwenye chupa sio whisky feki ila ilikuwa ni mkojo, adhabu aliyopewa haikuwa kifungo cha jela kama ambavyo wengi walitarajia, amefungiwa kufanya biashara ya kuuza vinywaji kwa miezi 2.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top