tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Stori Dustan Shekidele, Morogoro/Ijumaa
MSHIRIKI wa
Shindano la Miss Tanzania mwaka 2014, aliyeshinda taji hilo katika
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na baadaye kuthibitika kuwa
alighushi umri na hivyo kulitema na kusababisha kufungiwa kwa shindano
hilo, Sitti Mtemvu, juzikati alipokewa kama mfalme alipofanya ziara fupi
mjini Morogoro.
Mrembo huyo ambaye hivi sasa anaongoza taasisi yake inayofahamika kama
Sitti Tanzania 2015, alipofika mjini hapa, baadhi ya mashabiki wake
walijipanga kutokea eneo la Nanenane na kuambatana naye hadi katika
hospitali ya mkoa ambako alitoa msaada wa vyandarua katika wodi ya
wazazi.
Baada ya kukabidhi misaada hiyo, mrembo huyo ambaye baba yake mzazi ni
Mbunge wa Jimbo la Temeke, alikwenda hadi ofisi za Chama cha soka mkoani
hapa na kutoa msaada wa mipira mitano na seti moja ya jezi kwa lengo la
kusaidia kuimarisha michezo.
“Najisikia vizuri sana nimepokelewa kama mfalme, kundi la wananachi wa
Morogoro walijipanga maeneo ya Nanenane ambapo walinipokea, binafsi
sikutarajia kukutana na mapokezi kama haya, mimi ni Mluguru na nimekuja
kwetu Morogoro kuwasaidia watu wenye uhitaji mbalimbali,” alisema binti
huyo baada ya kumaliza shughuli zake.
Lakini katika hali ya kushangaza, alipoulizwa kuhusu anavyojisikia baada
ya kulitema Taji la Miss Tanzania, Sitti alijibu kwa mkato; “Sijisikii
vibaya na wala sitaki kuzungumza ishu ya Miss Tanzania,” alisema na
kukatisha mahojiano hayo hapohapo kabla ya kuingia kwenye gari lake bila
hata kumuaga mwandishi.
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment