Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

UNYAMA..!! MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA WILAYANI KAHAMA, WIVU WA KIMAPENZI WAHUSISHWA

tiko tiko

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..

Mwanamke mmoja aitwae Scholastika Shija (55) mkazi wa Mtaa wa Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kukatwa mapanga kichwani na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa Kimapenzi.

Akizungumza leo DUNIA KIGANJANI, afisa mtendaji wa Mataa huo, Rafael Jumanne amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo wakati Scholastika akiwa nyumbani kwake anajiandaa kulala akiwa na wajukuu zake wawili.

Jumanne amesema majambazi hayo ambao idadi yao haikufahamiaka, walianza kumcharanga Scholastika mapanga kichwani na mkono wa kulia hali ambayo ilisababisha kuvuja kwa damu nyingi na baadaye kifariki dunia.

Amesema chanzo cha mauji hayo bado hakijafahamika ingawa yanahusishwa na wivu wa kimapenzi na kwamba jeshi la Polisi limefika eneo la Tukio na kuupeleka mwili wa maraehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Jumanne amesema Mbali na watu hao kufanya mauaji hayo, pia waliiba baiskeli moja, huku kukiwa hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kwamba watashirikiana na jeshi la Polisi kufanya upelelezi.

Akizumgumza kwa njia ya Simu na Kahama FM Kamanda wa Polisi mkoa wa Shimyanga Justus Kamugisha amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi unaendelea kufanyika ili kuwabaini na hatimaye kuwafikisha katika sheria.

Kamanda kamugisha amewataka wananchi kuacha kuamini imani za Kishirikina ambazo kimsingi zinaleta uchochezi wa mauaji ya vikongwe huku akiitaka jamii ishirikiane na jeshi la Polisi kuwafichua waliohusika.

Na Ndalike Sonda - Dunia Kiganjani> Kahama

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu

tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top