tiko
tiko
WAKATI diva
wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’ akielezwa kuwa mambo yake hivi
sasa yako kwenye mstari kwa kusajili kampuni yake ya mambo ya sinema,
mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Pamela ameibuka na kumtaka
muigizaji huyo kuacha kumfuata mume wake, Amani lina data kamili.
Mwanamama huyo, anayefanya kazi ‘nzuri’
katika shirika moja kubwa nchini, aliliambia gazeti hili kuwa Kajala,
amekuwa akitembea na mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Tanaluza ambaye
kwa sasa yuko ndani katika gereza la Keko kwa kosa ambalo alikataa
kulitaja.
“Jamani namtahadharisha Kajala, asije
kunikuta pale, patakuwa hapatoshi, yeye si hodari wa kwenda kuangalia
waume za watu, awe na haya, aende Ukonga akamuangalie mumewe, ushauri wa
bure nampa,” alisema Pamela kwa jazba.
Alisema anazo taarifa kuwa Kajala
alikuwa akitembea na mumewe kabla hajapatwa na matatizo na baada ya
kupelekwa Keko gerezani, amekuwa akienda hapo kwa kujifichaficha, kitu
ambacho alisema siyo kizuri kwa sasa, kwani anaweza kumsababishia mumewe
matatizo zaidi.
“Huyo ni mume wangu, ananihitaji kwa
hali na mali sasa hivi, nisije nikaacha kwenda kwa ajili ya Kajala, kama
aliwahi kumpangishia nyumba ya kifahari na kumnunulia gari, ni huko
huko, sasa hivi anahitaji kuwa na mimi mkewe, kwanini yeye asiende kwa
mume wake na yeye si amefungwa?,” alihoji Pamela.
Baada ya maelezo hayo kutoka kwa mke,
gazeti hili liliingia mtaani kwa nguvu kumsaka Kay, ambaye mume wake,
Faraja Augustino amefungwa jela miaka saba kwa kosa la utakatishaji
fedha na kufanikiwa kumpata kupitia simu yake ya mkononi.
“Mimi mbona simjui huyo mwanaume, wala
sijawahi kufika huko keko, kama anatafuta umaarufu kupitia jina langu
aseme, asinisingizie,” alisema Kajala baada ya kusomewa mashtaka yake,
majibu ambayo licha ya kuyaheshimu, lakini gazeti hili linaendelea na
uchunguzi wake ili kubaini ukweli zaidi.
tiko
tiko
Post a Comment