tiko
tiko
Wenyeviti wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), leo watakutana kwenye mkutano wa faragha kwa ajili ya
kujadili ajenda mbalimbali zinazohusu mustakabali wake na hali ya
kisiasa nchini.
Wenyeviti hao, Freeman Mbowe (Chadema),
James Mbatia (NCCR Mageuzi), Emanuel Makaid (NLD) na Profesa Ibrahim
Lipumba (CUF) wanakutana kwenye mkutano huo ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa kalenda ya Ukawa.
Juhudi za kuwapata viongozi hao ili
kuthibitisha ziligonga mwamba lakini Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi Bara,
Mosena Nyambabe alisema jana kuwa mkutano huo utafanyika kama
ilivyopangwa.
“Ninachofahamu mkutano huo lazima
utafanyika lakini siwezi kujua utafanyikia wapi kwa hapa Dar es Salaam
kwani ratibu zote wanazifahamu viongozi wenyewe,” alisema Nyambabe.
Awali, Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James
Mbatia alimwambia mwandishi kuwa mkutano huo utakuwa na ajenda
mbalimbali likiwamo suala la kuangalia mgombea wa nafasi ya urais
kupitia umoja huo.
Ajenda nyingine alizotaja ni kura ya
maoni ya Katiba Inayopendekezwa, changamoto ya uandikishaji wa Daftari
la Mpigakura, hali ya uchumi na tathmini ya uchaguzi wa Serikali za
Mitaa uliomalizika mwishoni mwa mwaka jana.
Mbatia alisema: “Ajenda hizo
tunazijadili na lengo ni kuhakikisha tunatafuta majibu ya changamoto
mbalimbali zilizopo kwa sasa,” alisema na kuongeza:
“Kuhusu suala la mgombea urais wa Ukawa, linaweza kuwa sehemu ya mazungumzo lakini halipo kwenye ajenda.”
Mbali na ajenda hizo, mwongozo wa umoja
huo imekuwa ni jambo linalodaiwa kuwa changamoto katika utekelezaji
wake. Kuhusu maandalizi ya mwongozo wa umoja, Mbatia alisema suala hilo
pia litakuwa sehemu ya ajenda hizo.
tiko
tiko
Post a Comment