tiko
tiko
Mzoga wa mamba mwingine. Mzee aliyewatega mamba hao (aliyeketi) akiwa nyuma ya mzoga wa mamba mmojawapo. Mwanakijiji akiweka pozi juu ya mzoga wa mamba kuonesha furaha yake.
WANAKIJIJI wa
Kome-Mchangani wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wamewaua mamba wawili
wanaodaiwa kuua watu wawili na kuwajeruhi watu watatu.
Mamba hao waliokuwa katika kingo za Ziwa
Victoria kijijini hapo, walitajwa kuwa kero kubwa kiasi cha kusababisha
baadhi ya shughuli za kuinua uchumi katika kijiji hicho kama vile uvuvi
na umwagiliaji kusimama kwa muda huku wanakijiji wakiwa na hofu ya
kuliwa na mamba hao.
Wakizungumza na mwandishi wetu,
wanakijiji hao walidai kuwa mara kadhaa walifikisha malalamiko yao kwa
viongozi wa serikali lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, jambo
lililowafanya wachange pesa na kumpa mzee mmoja ambaye alitumia mbinu za
kitaalamu kuwatega mamba hao na hatimaye kuwaua.
tiko
tiko
Post a Comment