tiko
tiko
Mali za Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba
Mali
za Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba zimetangazwa kupigwa
mnada kutokana na kushindwa kulipa deni analodaiwa na Benki ya CRDB.
Mali
hizo zinahusisha eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 2,214 lililopo
Mbezi Tangi Bovu, Dar es Salaam, kiwanja namba 1030 kilichosajiliwa kwa
jina la John Damiano Komba na Salome Komba.
Kwa
mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari, Kampuni ya
Uwakili ya Mpoki & Associates Advocates inayoiwakilisha CRDB
imetangaza kuuza eneo hilo la kibiashara lililotengwa kwa ajili ya
ujenzi wa vituo vya mafuta, maduka makubwa, benki, sehemu ya kufanyia
mazoezi, hospitali na huduma nyingine za kijamii.
“Tayari
eneo hilo lina nyumba kubwa ya kuishi upande unaotazamana na barabara
mpya ya Bagamoyo. Kwa upande wa kusini mwa jengo kuu linalotazama
barabara hiyo kuna nyumba nyingine ya kuishi, fremu za maduka na ofisi,”
ilisomeka sehemu ya tangazo hilo.
Alipoulizwa
juu ya gharama halisi anazodaiwa Kapteni Komba na muda wa deni hilo,
mmiliki wa Kampuni ya Mpoki & Associates Advocates inayoratibu mnada
huo, Mpale Mpoki alisema maelezo yote yanayohusu kiasi cha mkopo na
muda wa deni yatajibiwa na CRDB wenyewe.
Hata
hivyo, uongozi wa CRDB haukupatikana jana kuzungumzia suala hilo na
Kapteni Komba alipoulizwa alisema hakuna jambo kama hilo... “Hakuna kitu
kama hicho, waulize hao waliotoa
tiko
tiko
Post a Comment