tiko
tiko

Mwigizaji wa filamu za Kibongo Jennifer
Kyaka ‘Odama’, amedai kuwa mwanaume ambaye anaweza kumuoa jambo la
kwanza lazima atambue kuwa yeye anafanya filamu kwa muda mrefu hivyo
hawezi kuacha kazi yake kwa sababu ya kuingia kwenye ndoa.
Odama alifungua kinywa chake baada ya
kuzungumza na paparazzi wa GPL, ambapo alidai kuwa haiwezi kutokea
kuacha kufanya filamu ili amridhishe mwanaume kwani maisha yake yamekuwa
yakiendeshwa na kazi hiyo kwa muda mrefu.
“Naamini kuwa yule ambaye atakuja kwa
nia ya kunioa kwanza lazima atambue kuwa nafanya filamu, sitahitaji
anieleze jambo la kuacha kazi yangu, mimi ni mwanamke ambaye nahitaji
kupata maendeleo kupitia kazi zangu,” alisema.
Picha:Odama akiwa na mtoto wake.
tiko
tiko
Post a Comment