tiko
tiko

Ukimuona mtu mzima ujue kapitia mengi
kisome hapa kisa cha mrembo na mwigizaji wa filamu hapa Bongo, Esha
Buheti kuungua na moto miguuni. Esha anaeleza..
Tarehe kama ye leo (jana) nikiwa nipo
darasa la nne nakumbuka nimetoka shule nikawa naenda mtoni kuchota maji ,
wakati naelekea mtoni njiani nikaona sehemu imetulia kuna kama mchanga
mweupeee kwakua nilikua sijui akili ikaniambia ule ni mchanga wa beach.
Nikaacha kufata maji nikaenda mpaka pale
kwenye ile sehemu nikawa najiuliza hiki nini wakati natafakari,
nikajikuta naanza kutembea kuelekea kwenye ule mchanga kumbe haikua
mchanga ilikua jivu la moto lililotakana na mapumba ya mpunga
yaliochomwa bila kujua nkawa naendelea kumbe mbele kuna shimo lenye
mapumba yenye moto nikadumbukia nikaanza kuskia maumivu ya moto
nikaungua sana miguu yangu......

Niliungua vibaya sana niliuguzwa vidonda
vikapona baada ya mwezi mzima..... Ila makovu yalibakia miguuni mwangu
kuna siku nipo mitaa ya Mwenge(Dar) natengeneza kucha akapita Mmasai
akaniona akanambia ana dawa yakutoa makovu ya moto sikumuamini, ila
akaniambia itakuponya basi nikanunua nikaanza kutumia .
Leo hii naitazama miguu tangu hata
siamini.......(Kama inavyoonejkana kwenye picha hapo juu) Ila kuna kovu
bishiii ilooo limegoma kutoka but naridhika na hali yangu niliokua
nayo.....
Esha alimalizia na msemo huu.
“Ridhika na ulichojaaliwa nacho Mungu ila jifunze kua kama upo hai jua kabisa bado unaendelea kuumbwaa”.
Pole sana, Ujumbe umefika.
tiko
tiko
Post a Comment