tiko
tiko
MWIMBAJI nyota
wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando ambaye hivi karibuni alikanwa
na aliyewahi kuwa meneja wake wa muda mrefu, Alex Msama, anadaiwa
kuweweseka asijue la kufanya kufuatia hatua hiyo.
Akizungumza kutoka Dodoma yalipo makazi
ya mwimbaji huyo, mmoja wa watu wake wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina
lake, alisema hatua ya Msama kutangaza kutofanya naye kazi, limekuwa
pigo kwake kwani ndiye aliyekuwa kiongozi na mwokozi wake wa mambo mengi
ya kikazi na binafsi.
Meneja wa Rose Mhando, Alex Msama.
“Anaweweseka kwa kweli na hajui la
kufanya, Msama ndiye alikuwa msaada wake mkubwa kwa kila kitu kuhusiana
na muziki japo kwa sasa amekuwa hataki hata kumsikia Rose,” alisema mtu
huyo.
Rose alipigiwa kutaka kusikia kutoka
kwake, lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa
ujumbe mfupi ulionyeshwa kupokelewa bila majibu. Msama alipoulizwa
kuhusu kilio cha msanii huyo alisema yeye ameshatoa msimamo wake na
unaeleweka.
tiko
tiko
Post a Comment