tiko
tiko
Serikali
ya Malaysia imetangaza kusitisha shughuli ya kuitafuta ndege iliyopotea
ya MH370 na kusema wanachukulia kama ajali ambayo iliangamiza watu
wote.
Tangu kuanza kutafutwa kwa ndege hiyo iliyopotea tangu March 8 mwaka 2014 wakati ikitokea Malaysia kuelekea China hakukuwahi kuwa na dalili yoyote ya kupatikana kwa watu wala kitu chochote kilichokuwa kwenye ndege hiyo.
Maafisa wakuu wanasema shughuli ya
kuitafuta ndege hiyo bado inaendelea lakini wanahisi kwamba abiria 239
waliokuwa kwenye ndege hiyo wote walifariki.
Hata hivyo Maofisa wa Serikali wa nchini
hiyo walitoa taarifa leo na kusema ndugu na jamaa wa waathirika wa
ndege hiyo watalipwa fidia.Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment