tiko
tiko
JESHI la polisi nchini Kenya
limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi wa Shule ya
Msingi Lang'ata iliyopo jijini Nairobi walioandamana kupinga kitendo
cha kunyanganywa uwanja wao wa michezo uliouzwa kwa mwekezaji binafsi.
Polisi hao wakiwa na mbwa waliwatawanya
wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka
sita baada ya kuangusha ukuta mpya uliojengwa kutenga shule yao na
Uwanja.
Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni
Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma na
kukuta kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walio kati ya umri wa miaka mitatu na 14 na inasimamiwa na Halmashauri ya Jiji.
Wanafunzi kadhaa wamejeruhiwa katika
purukushani hizo wakati polisi walipoingilia kati na kujaribu
kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wanazua vurugu.
Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogomadogo.
Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wakiwa wamebeba fimbo ambapo polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa kwa mawe.
(PICHA / HABARI: BBC)
tiko
tiko
Post a Comment