Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

MWENYEKITI HALMASHAURI KYELA ADAIWA KUWAANDAA VIJANA KUWAFANYIA FUJO AKINA MWAKYEMBE

tiko tiko

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Gabriel Kipija, ameingia matatani baada ya kudaiwa kuandaa vijana waliowafanyia vurugu wabunge wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipofanya ziara wilayani humo.

Waliofanyiwa vurugu hizo ni pamoja na  Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi.


Kipija ambaye ni Diwani wa CCM kata ya Kyela mjini anadaiwa kuwaanda vijana hao mwishoni mwa mwaka jana na kwamba waliandika mabango yenye ujumbe wa  kuilaumu serikali na mbunge wa Kyela kwa kushindwa kuboresha miundombinu.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kyela, Dk. Hunter Mwakifuna, akizungumza katika mahojiano ili kujua ukweli wa suala hilo,  alisema chama kilishapokea malalamiko kuhusiana na kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti huyo na taratibu za chama zinaendelea kufanywa kuangalia hatua za kuchukua.


 “Malalamiko dhidi ya Kipija chama kilishayapokea na kimekaa vikao kujadili suala hilo na mtuhumiwa kuitwa na baada ya hapo hatua zinazostahili kuchukuliwa zitafanywa kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za chama,”alisema.


 Dk. Mwakifuna alisema  kama itathibitika mwenyekiti huyo alifanya njama hizo atakuwa na kosa  kubwa kwa sababu  kama kiongozi ana nafasi kubwa ya kufikisha suala lolote ngazi ya wilaya anapoona kuna mradi au jambo lolote la maendeleo haliendi vizuri badala ya kuandaa vijana kufanya vitimbi.


Kipija pia analalamikiwa kukisaliti chama wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kusaidia vyama vya upinzani ili viweze kupata ushindi.


Kwa upande wake Katibu wa CCM Kata ya Kyela Mjini, Yohana Mnongo, alisema vikao vya chama ngazi ya kata kikiwamo cha maadili kilishakaa kujadili tuhuma zinazomkabili Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Kipija.


Mnongo alisema katika hatua ya awali vikao hivyo vilishawasilisha mihtasari ya mambo yaliyojadiliwa katika ngazi ya wilaya kama taratibu za chama zinavyoeleza.  


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Kipija, akizungunza shutuma hizo alikiri kuandaa makundi ya watu ambao waliandika mabango kwa kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa wabunge hao ambao kamati yao inasimamia suala la miundo mbinu.


Alisema hatua ya kuandaa watu hao ilitokana na kwamba barabara za Kyela- Matema na Ibanda-Itungi port zimejengwa chini ya kiwango na kila anapolifikisha suala hilo kwa viongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kupitia vikao vya Bodi ya Barabara ya Mkoa linapuuzwa.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top