tiko
tiko
MFANYABIASHARA mwanamama
aliyetambulika kwa jina la Prisca Paul Rugeiyamu au Mama Koku (34)
ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi nje ya geti la nyumba yake huku
mwanaye Careen (12) akishuhudia.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea
Januari 12, mwaka huu saa mbili usiku maeneo ya Tabata Segerea jijini
Dar ambapo kwa mujibu wa chanzo, Prisca alikuwa akirejea nyumbani kwake
ndani ya gari aina ya Vitz baada ya kukusanya mapato yake ya siku kutoka
kwenye biashara zake.
Akiwa nje ya geti la nyumba yake
akisubiri kufunguliwa, ndipo majambazi walitokea ghafla wakiwa kwenye
pikipiki na kulizunguka gari hilo na kutoa bastola wakitaka wapatiwe
fedha na laini za mitandao ya simu alizokuwa akizitumia katika biashara
yake ya huduma za kifedha kwa njia ya simu katika moja ya maduka yake.
Chanzo hicho kilisema kuwa, Prisca
alibishana na majambazi hao kwa muda ambapo walimpiga risasi ya mguuni
na kumuongeza nyingine baada ya kuendelea kugoma kutoa fedha.
“ Walimpiga risasi nyingine sehemu za tumbo na kuchukua fedha zinazodaiwa kufikia shilingi milioni arobaini na tano huku mwanaye Careen akishuhudia tukio hilo baada ya kufungua geti hilo kwa ajili ya kumpokea mama yake,” kilisema chanzo.

Inaelezwa kuwa Careen baada ya kuona
hayo alikimbilia kwa bibi yake ambaye ni mama mzazi wa Prisca anayeishi
jirani na nyumba yao aliyefika eneo la tukio ambapo majambazi hao
waliokuwa wakijiandaa kutoweka walimpiga risasi ya mguu mama huyo na
kuondoka kwa kasi.
Hata hivyo, baada ya majirani kufika
eneo hilo walimchukua Prisca na kumkimbiza Hospitali ya Amana lakini
alifariki akiwa njiani na maiti yake ikahifadhiwa hospitalini hapo.
Akizungumza na waandishi wetu, ndugu wa
familia hiyo anayejulikana kwa jina la Geofrey Frank alisema kuwa baada
ya kifo chake walishangaa kuona wafanyabiashara wa madini wakija katika
msiba na kudai kuwa Prisca alikuwa mfanyabiashara mwenzao, na kuongeza
kuwa marehemu hakuweka wazi kazi yake hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo marehemu alikuwa mfanyabiashara wa madini, mmiliki wa duka la vocha za jumla, duka la vifaa vya ujenzi na mmiliki wa duka la vinywaji maeneo ya Segerea.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo marehemu alikuwa mfanyabiashara wa madini, mmiliki wa duka la vocha za jumla, duka la vifaa vya ujenzi na mmiliki wa duka la vinywaji maeneo ya Segerea.
Amewaacha yatima watoto watatu, mkubwa
ana miaka 12 huku wengine ni mapacha wana miaka saba. Mwili wa marehemu
ulizikwa Januari 15, mwaka huu katika Makaburi ya Segerea jijini Dar.
Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Deogratius Mongela na Chande Abdallah.
Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Deogratius Mongela na Chande Abdallah.
tiko
tiko
Post a Comment