tiko
tiko
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Phillipo Kalangi.
MFANYABIASHARA
wa kuuza samaki, Mkome Marwa (39) wa mtaa wa Nyasura wilayani Bunda,
ameuawa na watu wasiojulikana baada ya kupigwa risasi njiani akiwa na
mke wake, huku mwingine akijeruhiwa katika matukio mawili tofauti wilaya
humo.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mara, Phillipo Kalangi, amesema tukio la kwanza
limetokea Januari 12 mwaka huu, saa 3 usiku, eneo la Nyasura wakati
Marwa akiwa na mkewe wakirejea nyumbani kwao, amepigwa risasi na mtu
asiyefahamika.
Hata
hivyo, Kilangi amesema mtu huyo baada ya kufanya tukio hilo hakuweza
kuchukua kitu chochote kwa mfanyabiashara huyo aliyefariki hospitali ya
rufaa Bugando, Mwanza wakati akipatiwa matibabu, huku ofisi yake ikituma
makachero wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina.
Amesema
baada ya mfanyabiashara huyo kupigwa risasi, akajikokota hadi nyumba ya
jirani walikojifungia ndani ya geti na mkewe, hali iliyomfanya muuaji
kuwafuata tena lakini alipokuta geti limefungwa, akaondoka zake.
Tukio
la pili amesema limetokea siku hiyo saa 4:00 eneo la Bunda Day, wakati
mwanaume mmoja, Ndaro Malemi (25), aliyekuwa anaelekea nyumbani kwake,
alijeruhiwa kwa risasi na mtu asiyefahamika ambaye pia hakuchukua kitu
chochote.
Malemi
aliyelazwa katika hospitali ya DDH-Bunda, alisema mtu huyo aliyevaa
koti jeusi alimvizia njiani na kumwamuru atoe kila kitu na baada ya
kukimbia ndipo alipomiminiwa risasi mbili na kutokomea zake
kusikojulikana.
Daktari
wa zamu katika hospitali hiyo, Dk. Amosi Manya, amesema waliwapokea
majeruhi wawili hospitalini hapo lakini mmoja alikuwa na hali mbaya na
kukimbizwa Bugando lakini alifariki akiwa anapatiwa matibabu.
tiko
tiko
Post a Comment