tiko
tiko
DUNIANI kuna matukio! Tofauti
na utaratibu uliozoeleka, katika hali ya kushangaza, wanandugu
wamelazimika kusafirisha maiti juu ya keria ya basi kutoka Arusha hadi
Lushoto, Tanga kutokana na ukata.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo chanzo kilieleza kuwa, wanandugu hao ambao hawakuwa tayari kuanika majina yao, walifikia hatua hiyo ili waweze kuenea kwenye basi moja aina ya Toyota-Coaster kwenda Lushoto, mkoani Tanga.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo chanzo kilieleza kuwa, wanandugu hao ambao hawakuwa tayari kuanika majina yao, walifikia hatua hiyo ili waweze kuenea kwenye basi moja aina ya Toyota-Coaster kwenda Lushoto, mkoani Tanga.
Waombolezaji wakiupandisha mwili wa marehemu (ndani ya jeneza) juu ya gari.
“Waliona kama wangeweka maiti ndani ya
gari, wangelazimika kutoa siti mbili hivyo wasingetosha, baadhi ya ndugu
walishauri kwamba mwili wa marehemu uwekwe juu ya keria ili
waombolezaji waweze kuenea,” kilisema chanzo.
Chanzo hicho kilizidi kushusha data
kuwa, kabla ya wanandugu kukubaliana kusafirisha juu ya keria mwili huo,
uliibuka ubishani mkubwa kwani kuna baadhi waliafiki kitendo hicho
lakini wengine hawakuafiki.“Kuna ambao walikataa na kusema si jambo la
busara kuiweka maiti juu ya keria lakini mwisho wa siku walizidiwa kwa
hoja na wale walioshauri iwekwe juu kwani tatizo lilikuwa kwenye fedha
za kukodi gari jingine.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwekwa vizuri kwenye keria ya gari tayari kwa safari.
“Walishajikusanya kusanya hadi dakika za
mwisho, fedha walizopata zilitosha kukodi gari moja hivyo hawakuwa na
jinsi japo ambao hawakuafiki, walihofia kuwa huenda wasifike salama huku
wengine wakichungulia pembeni kila wakati wakihofu huenda jeneza
linaweza kuanguka,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo pamoja na kutofautiana huko
kwa wanandugu, walifanikiwa kusafiri salama hadi Lushoto na kufanikiwa
kumpumzisha mpendwa wao.
tiko
tiko
Post a Comment