tiko
tiko
Katika kile kinachoonekana
waigizaji wa kike kutaka kukuza tasnia ya uigizaji kwa kuvuka mipaka ya
nchi, mwigizaji Irene Uwoya amesema kuwa anataka atambulike nje ya nchi
kuliko ndani.
Akiweka hoja yake sawa, mwanadada
huyo anayedaiwa kuendelea kuwa na mvuto katika tasnia ya filamu alisema
anajua kuwa siyo jambo rahisi kufanya vizuri nje ya nchi, lakini huko
ndiko anakotaka kufika, hivyo inyeshe mvua au liwake jua, atajitahidi
kuhakikisha kwamba ndoto zake zinatimia.
Uwoya alisema kuwa alijaribu
kutengeneza mtandao wa kazi na wasanii wa nje wakati anatayarisha filamu
ya ‘Kisoda’ ambayo picha zake zilipigwa nchini Afrika Kusini na
Uturuki. Alifafanua kama wakati mwingine siyo lazima kusafiri, kuna
wakati wasanii wa nje wanaweza kuja Tanzania kikazi, ujio wao ni nafasi
ya pekee kwao, au kwa kufanya nao kazi hapahapa, ama kuchukua
mawasiliano na kuwafuata baadaye kwa ajili ya kufanya nao kazi.
“Tena nawaambia wale wote wenye
nafasi au wanaofahamiana na watu wanaopenda kwa dhati kufanya kazi na
waigizaji wa Tanzania, wasikose kuwaambia hata mimi napenda na ninaweza
kufanya hivyo, ”alisema Uwoya.
Mwigizaji huyo alifafanua kuwa njia
pekee ya kutangaza kazi za ndani Kimataifa ni kufanya kazi na waigizaji
wa nchi nyingine ambao watakuwa na hamu ya kukufuatilia na kufuatilia
kazi zetu nyingine pia. Aliongeza kuwa kwenye muziki angalau kuna
mwanga, lakini kwenye uigizaji bado juhudi inahitajika kwani baada ya
kufariki dunia kwa mwigizaji Steven Kanumba, mbio za kujitangaza kama
zimefifia.
Kauli hiyo ya Uwoya imekuja wakati
waigizaji kadhaa wakionyesha nia kama yake akiwamo Wastara anayenadi
filamu mpya ya ‘Mateso wanayopata Watanzania nje ya nchi’ na mwigizaji
anayedaiwa kuwa na nguvu ya kukubalika kwenye jamii Wema Sepetu akiwa
amerudi juzi kutoka nchini Ghana ambako alikwenda kupiga picha za filamu
yake iitwayo ‘After Death’.
tiko
tiko
Post a Comment