tiko
tiko
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa Jamhuri kufanya marekebisho ya hati ya mashitaka katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee (35) na wenzake wanane.
Hakimu
Mkazi Janeth Kaluyenda alitoa amri hiyo jana wakati akitoa uamuzi wa
ombi la washitakiwa hao kufutiwa mashitaka. Akitoa uamuzi huo, Hakimu
Kaluyenda alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili na kupitia kesi
mbalimbali hivyo aliamuru hati ya mashitaka ifanyiwe marekebisho ndani
ya siku saba.
Katika
ombi lao washitakiwa kupitia kwa Wakili wao Peter Kibatala waliiomba
Mahakama iwafutie mashitaka ya kufanya mkusanyiko usio halali kwa lengo
la kutembea kwenda kwenye Ofisi ya Rais kwa kuwa lina mapungufu
kisheria.
Washitakiwa
hao wanakabiliwa na mashitaka, wakidaiwa Oktoba 4, 2014 katika Mtaa wa
Ufipa, bila kuwa na uhalali walikiuka amri halali ya kutawanyika
iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf kwa niaba ya Jeshi
la Polisi
tiko
tiko
Post a Comment