Saa chache zilizopita tabasamunadaniel.blogspot.com ilipata taarifa kwamba kuna ajali iliyotokea eneo la Survey, Dar es Salaam jirani na Mlimani City.
Nimekuwekea picha za eneo la tukio, gari
mbili zimeangukiwa na mti mkubwa katika eneo hilo, ni mtu mmoja tu
aliyepata jeraha mguuni ambapo alipata jeraha hilo baada ya kujigonga
kwenye chuma alipokuwa akijaribu kukimbia wakati mti huo ukiwa
unaanguka.
Hapa kuna picha nilizokupigia muda mfupi baada ya kutokea tukio hilo.
Gari ya Askari wa Usalama Barabarani wakiwa eneo la tukio.
Moja ya gari ndogo ambayo iliminywa na mti huo.
Gari zikipita kwa tabu katika eneo hilo baada ya mti huo kuanguka.
Askari akichukua maelezo ya mwenye gari ambayo imeangukiwa na mti.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia
kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote
kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
Post a Comment