tiko
tiko
Kijana Iddy (mwanafunzi wa UDOM), aliyevunjika mguu katika vurugu za mgomo uliyofanywa na wanafunzi wa UDOM juzi.Mguu wa kulia wa kijana Iddy ukiwa umevunjika.
KIJANA Iddy ambaye ni mwanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyevunjika mguu katika vurugu za mgomo
uliofanywa na wanafunzi wa UDOM Kitivo cha Sayansi ya Jamii juzi
amepatiwa msaada wa matibabu na baskeli ya kutembelea walemavu 'wheel
chair'.
Iddy ambaye amelazwa katika Hospitali ya
General Dodoma, jana alipatiwa msaada wa fedha za matibabu pamoja na
'wheer chair' kutoka kwa Mhe. Shabiby baada ya kuzuiliwa kutoka
hospitalini hapo kutokana na deni kubwa la matibabu aliyokuwa anadaiwa.
Mzazi wa kijana huyo ameeleza kuwa
aliambiwa atapata msaada kutoka chuoni lakini cha kushangaza mpaka jana
jioni alikuwa hajapata msaada wowote kutoka chuo cha UDOM zaidi ya
kupigwa chenga na huku baadhi ya viongozi wakitupiana mpira.
Baba mzazi wa kijana huyo ametoa
shukrani za pekee kwa Mhe. Shabiby aliyeguswa na kumsaidia kijana wake
ambaye kwa sasa anaendelea vizuri.
tiko
tiko
Post a Comment