Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

JUMUIYA YA WANAFUNZI WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU(TAHLISO) YAPINGA VIKARI WANAFUNZI UDOM KUFUKUZWA

tiko tiko

Mwenyekiti wa zamani wa TAHLISO, Mussa Mdede

JUMUIYA ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Nchini (TAHLISO) imeeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha kufukuzwa na kusimamishwa masomo baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 


Katika kile alichosema ni kulaani kitendo hicho, Mwenyekiti wa Tahliso, Musa Mdede aliomba serikali kuwarejesha chuoni wanafunzi hao ambao ni Waziri Mkuu wa Wanafunzi, Phillipo Mwakibinga na Rais wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Masatu Kyabwene waendelee na masomo yao.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, alisema wanafunzi hao kama viongozi walikuwa wakitekeleza wajibu wao wa kuwatetea wanafunzi wenzao wanaowaongoza ambao wanaishi maisha magumu kwa kuwa Serikali ilikuwa haijawapa mikopo.


Pia wamelaani askari Polisi kuwapiga na kuwajeruhi wanafunzi wa chuo hicho Januari 14, mwaka huu wakiwa kwenye maandamano wakitoka chuoni kwenda kumwona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda au Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.


Alisema walipanga kuwaona viongozi hao ili kuwaeleza malalamiko ya wanafunzi wa Stashahada ya Ualimu wa Masomo ya Sayansi ambao Serikali iliahidi kuwapa mikopo.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top