tiko
tiko
Huu unaweza kuwa mwaka wa mafanikio zaidi kwa mastaa wengi Tz, tumeona Jokate akisign deal ya kufanya biashara kubwa itakayomzalishia zaidi ya bil 8 za kitanzania chini ya lebo ya Kidoti, safari hii ni zamu ya staa mwingine, Vanessa Mdee leo kuna story nzuri inayomhusu mtu wangu!
Kampuni ya Samsung ni
kampuni maarufu kwa kuuza bidhaa mbalimbali, simu za mkononi ni moja ya
bidhaa hizo, leo January 16 Vee Money ameingia mkataba wa kuwa Balozi wa
bidhaa za Samsung.
Vanessa na uongozi wa kampuni ya Samsung wameingia makubaliano rasmi ya kufanya kazi pamoja, staa huyo ataanza kuonekana kwenye matangazo ya bidhaa za kampuni hiyo.
”Samsung ni
kampuni kubwa na yenye hadhi ya juu, ni heshima kubwa sana kwangu kuwa
Balozi wa kampuni hii inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya
Kieletroniki ulimwenguni , huu ni mwanzo tu wa jinsi mwaka 2015
utakavyokuwa na mafanikio kati yangu na kampuni ya Samsung, binafsi natumaini juu ya kazi hii na nasubiri kwa hamu siku nitakayoanza kazi rasmi“– Vanessa Mdee.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment