tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha
Askari
wa jeshi la wananchi Tanzania Benard Mdika (29) mkazi wa Old
Shinyangaamefariki dunia papo hapo baada ya pikipiki aliyokuwa
anaendesha kugongwa na gari lisilofahamika namba wala mmiliki wake
katika barabara ya Old Shinyanga eneo la shule ya sekondari KOM iliyopo
katika kata ya Lubaga manispaa ya Shinyanga usiku wa kuamkia leo .
Katika ajali hiyo wa skari wa jeshi hilo Nicholaus Donald(29) mkazi wa Old Shinyanga aliyekuwa abiria katika pikipiki hiyo ameumia usoni na kichwani na amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi wa dereva wa gari na jeshi la polisi linaendelea na juhudi
za kulifafuta gari husika na dereva.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment