tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Dar es Salaam. Wakati
CCM ikisubiri Februari kufanya tathmini kuona kama baadhi ya wagombea
wake wa urais wametekeleza masharti ya adhabu zao, washindani wao wa
Ukawa, Jumanne ijayo watakutana kujadili mambo mbalimbali, ukiwamo
mchakato wa kuwapata wagombea wake wa urais, ubunge na udiwani,
imefahamika.
Tangu mwaka huu uanze
zimekuwapo pilikapilika nyingi za kisiasa ndani ya vyama vya siasa na
Jumanne iliyopita CCM ilifanya kikao cha Kamati Kuu mjini Zanzibar na
kutoa maazimio yanayogusia mchakato huo lakini ikasita kutaja ratiba
rasmi ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM.
Wakati hali ikiwa hivyo,
habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya viongozi wa Ukawa,
umoja huo utakutana jijini Dar es Salaam Januari 20, ukiwa na ajenda
mbalimbali kuhusu ushirikiano wao, likiwamo suala la kupata wagombea
huku vikao vya ndani ya vyama vikitarajiwa mwishoni mwa mwezi huu.
Mwenyekiti Mwenza wa
Ukawa, James Mbatia alithibitisha jana kuwapo kwa kikao hicho Jumanne
akisema kutakuwa na ajenda nyingine lakini: “Suala la kupata wagombea
nalo huenda likajadiliwa. Kuhusu suala la mgombea urais wa Ukawa,
linaweza kuwa sehemu ya mazungumzo lakini halipo kwenye ajenda.”
Ajenda nyingine
alizotaja ni mwongozo wa Ukawa, kura ya maoni ya Katiba, changamoto za
uandikishaji wa daftari la wapigakura, hali ya uchumi na tathmini ya
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliomalizika Desemba mwaka jana. Mbatia,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alisema watajadili ajenda hizo
ili kuhakikisha wanatafuta majibu ya changamoto zilizopo kwa sasa.
Kiongozi huyo pia
alithibitisha taarifa kuwa kila chama ndani ya Ukawa kupitia vikao vyake
kitateua majina ya wagombea ambao watashindanishwa ndani ya umoja huo,
akisema kabla ya Machi, jina la mgombea urais ndani ya chama chake
litakuwa limeshapendekezwa.
Awali, Katibu Mkuu wa
NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema vikao vya chama hicho
vinavyotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu vitakuwa na ajenda ya
uchaguzi vitakavyojadili mwelekeo wa uchaguzi huo kama kalenda yake
inavyosema.
“Nadhani vikao hivyo
ndiyo vitaanza kujadili ajenda ya uchaguzi ujao. Tulishatoa nafasi ya
watu kujitokeza kwenye nafasi mbalimbali. Tukishapendekeza majina ya
wagombea kwa baadaye ndiyo tutawapeleka ili kuchambuliwa kwa pamoja na
kamati ya Ukawa.
“Mpaka sasa kamati ya
Ukawa inaendelea na kazi yake tangu Oktoba mwaka jana ila inakuwa vigumu
kwa wajumbe kujua kazi zote zinazofanywa na kamati hiyo kutokana na
msingi wa majukumu yake.”
Nyambabe alisema kamati
hiyo imekuwa ikifanya kazi, ikijumuisha wajumbe wasiopungua watatu
kutoka kila chama ili kufanya tathimini, kuchambua na kuratibu shughuli
zote za uchaguzi.
Kuhusu kupata mwongozo
wa Ukawa, Nyambabe alisema: “Namna ya kupata mgombea, ilani moja na
mwelekeo, vinaweza kuonekana kuanzia Februari baada ya vyama kukaa vikao
vyake.”
Wakati Nyambabe akisema
hayo, kumekuwa na taarifa katika vyombo vya habari kuwa CUF
kimeshatangaza kumsimamisha Profesa Ibrahim Lipumba kuwania urais,
ambazo hata hivyo, zimekanushwa na Naibu Katibu Mkuu wake Bara,
Magdalena Sakaya.
>>> Mwananchi
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment