tiko
tiko
Gogo akiwa darasani na wanafunzi wenziwe.
Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa
Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita
inaaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi
duniani.
Akiwa ameketi dawati la mbele kabisa
darasani ,yuko darasa la tano na amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo
Sitienei anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa makini hukua akiandika
majina ya wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla alijiunga na shule hii ya
Leaders Vision Preparatory School miaka mitano iliyopita lakini pia
aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake cha Ndalat kilichoko kwenye
bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na mitano iliyopita.
Darasani Priscilla anawasaidia wengine
wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14 na mar azote
huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla anajulikana kama Gogo maana
yake bibi katika lugha ya jamii ya wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa
na umri wa miaka 90 katika umri huo anajua kuandika na kusoma pia fursa
aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha ambayo Priscilla anajiona yuko
huru kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin kuliko kiingereza,pindi
anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua kujiunga na shule katika umri
wake.
Sababu kubwa ambayo amekuwa akiitoa,ni
ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa umri wake anataka
awahamasishe watoto kupata elimu,kwani anawaona watoto wengi wakiwa
hawako shuleni na watoto hao wana watoto.
Gogo apitapo mitaani haoni shida
kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni katika muda wa masomo na
kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo anasema watoto hao humjibu kwamba
hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name huwaambia mimi ni mkubwa
sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na shule.
Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona
watoto wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura
hovyo mitaani,bila msaada wowote.kutokana na hali hiyo nataka
kuwahamsisha waende shuleni.
tiko
tiko
Post a Comment