tiko
tiko
Uongozi
wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) umeazimia kumfukuza chuo moja kwa moja
waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Philipo MWAKIBINGA na kumsimamisha
Rais pamoja na Katibu wa serikali hiyo.
Maazimio
hayo yanafuatia kikao cha Baraza la chuo kilichoketi jana jioni na
waliosimamishwa ni Kyabwene (Rais) na Ismail Chande (Katibu)
Viongozi
hao wanadaiwa kuchochea mgomo uliotokea jana chuoni hapo, uliohusisha
maandamano yaliyofanywa na wanafunzi wa stashahada ya ualimu kupitia
mpango maalum wa serikali kwa madai ya kuongozewa posho ya kujikimu
pamoja na madai ya kucheleweshewa posho ya chakula.
Kwa
upande wake Mwakibinga amekiri kupokea barua ya kufukuzwa chuo na
kuongeza kuwa baada ya kukabidhiwa barua hiyo ikiwa ni muda mfupi baada
ya kutoka polisi walikokuwa wanashikiliwa tangu jana, alitakiwa kutoka
nje ya maeneo ya chuo kuanzia muda huo na alisindikizwa na polisi hadi
nje ya maeneo ya chuo.
Amesema hatachoka kupigania ukweli na ataendelea kupigania haki za wanyonge mahali popote atakapokuwa.
Akizungumzia
na paparazi kuhusu tuhuma za kuchochea maandamano chuoni hapo,
Mwakibinga amesema kuwa yeye kama kiongozi alikuwa analazimika kuwasemea
wanafunzi hao ambao bado wako katika hali mbaya kutokana na kutokuwa na
pesa ya kujikimu kiasi cha kukosa pesa ya chakula na kula "makombo ya
mgahawani".
MWAKIBINGA aliwahi kusimamishwa chuo kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kuruhusiwa kurudi chuoni na kuendelea na masomo.
tiko
tiko
Post a Comment