tiko
tiko
Picha
hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino
Mlowola wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya
matukio mbalimbali ya uhalifu.
Alisema
mtoto Pendo aliporwa na watu wasiojulikana kwa kuvamia makazi yao usiku
wa Desemba 27, mwaka jana akiwa amelala pamoja na wazazi wake na kisha
kupora mtoto huyo na kutokomea kusikojulikana.
“Natoa
wito kwa yeyote atakayemwona mtoto huyo atoe taarifa katika kituo cha
Polisi ama kwenye ofisi za serikali za mitaa, vijiji na vitongoji,”
alisema Kamanda Mlowola.
Kamanda
Mlowola alisisitiza kuwa Polisi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa
imeimarisha juhudi za kumsaka mtoto huyo na kuomba wananchi kutoa
taarifa zitakazowezesha kupatikana kwake.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alitembelea kijiji hicho Januari 5,
mwaka huu na kuzungumza na wakazi wa kijiji hicho ambao alitoa siku tano
mtoto huyo awe amepatikana akiwa hai ama mwili wake lakini hadi sasa
mtoto huyo bado hajapatikana.
Baba
wa mtoto Pendo, Emmanuel Shilinde ni miongoni mwa watu wanoshikiliwa na
Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi ya namna mtoto huyo
alivyoporwa na watu wasiojulikana.
Watu
15 wenye ulemavu wa ngozi wameuawa mkoani Mwanza tangu kuibuka kwa
wimbi la mauaji dhidi yao nchini mwaka 2008 kutokana na imani za
kishirikina.
tiko
tiko
Post a Comment