tiko
tiko
ENEO la Mjohororoni wilayani Hai, mkoa wa Kilimanjaro jirani na uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kando ya barabara ya
Moshi/Arusha, linazidi kuwa na rekodi mbaya ya matukio ya mauaji.
Hapa ndipo
aliuawa mfanyabiashara bilionea wa madini aina ya Tanzanite Erasto Msuya
(43) kwa kupigwa risasi zaidi ya 10 kifuani mwaka juzi- na sasa miili
mitatu ya watu wanaodhaniwa kuwa wachimbaji wa madini hayo mkoani
Arusha, imeokotwa ikiwa na michubuko midogo na wengine damu ikitoka
Puani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, amethibitisha tukio lakini akaahidi kutoa taarifa kamili baadaye.
Paparazi limeelezwa kuwa tukio hilo limetokea leo asubuhi majira ya 2:000 katika eneo hilo maarufu kama kwa Wasomali.
Vijana hao wanaodaiwa kuwa na umri kati ya miaka 28 na 32 walikutwa katika eneo hilo na msamaria mwema ambaye baadaye alitoa taarifa kituo cha Polisi Bomang’ombe.
Mtoa taarifa
wetu, amesema kuwa miili hiyo baada ya kuondolewa eneo hilo na polisi,
ilipelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mawenzi kwa ajili ya
kuhifadhiwa lakini ilishindikana kutokana na chumba cha kuhifadhia maiti
kujaa.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment