tiko
tiko
MSANII wa
filamu Bongo, William Mtitu ameelezea jinsi alivyoteseka usiku kucha
kisha kukimbizwa hospitali na kulazwa kwa saa kadhaa baada ya kuzidiwa.
Akizungumza na Amani, Mtitu alisema kuwa
hali hiyo ilitokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria usiku wa
kuamkia Jumanne ndipo alipelekwa katika hospitali moja iliyopo maeneo ya
Magomeni Kagera, Dar alikolazwa.
“Yaani hali yangu ilikuwa mbaya, usiku
sikulala kabisa nimejua kweli malaria ni hatari lakini kwa sasa
naendelea vizuri baada ya kuwekewa dripu, namshukuru Mungu,” alisema
Mtitu.Msanii huyo aliongeza kuwa, anaamini hali yake ilikuwa mbaya kwa
kuwa ni nadra sana kusumbuliwa na malaria.
tiko
tiko
Post a Comment