tiko
tiko
MAPENZI bwana!
Mohamed Khalfan ambaye ni kikongwe wa miaka 78 mwenye ulemavu wa ukoma
na mkewe, Habiba Shomari (68) hivi karibuni waliwashangaza watu baada ya
kuamua kumwagiana mabusu hadharani.
Bw. Mohamed Khalfan(78) akimchumu mkewe, Bi. Habiba Shomari(68).
Tukio hilo lilijiri kwenye Kambi ya
Walemavu wa Ukoma ya Chazi iliyopo Kata ya Chazi wilayani Mvomero mkoani
hapa ambapo kulikuwa na kikao cha serikali za mtaa kutatua mgogoro wa
ardhi.Akizungumza na Amani huku akiwa na furaha, Mzee Khalfan alisema
ndoa yake na mkewe ina miaka 60, walifunga mwaka 1955 mkoani hapa
”Nampenda sana mpenzi wangu huyu.
Nilifunga naye ndoa mwaka 55, ila kwa bahati Mungu hakutujalia kupata
mtoto hata mmoja.“Lakini pamoja na kukosa mtoto hata wa dawa, tunaishi
na mwezangu katika mapenzi mazito. Kila siku namwona kama mchumba na
yeye ananiona kama mvulana mbichi kabisa,” alisema kikongwe huyo mwenye
meno ya kuhesabu na kuwafanya watu wawapongeze hasa ikizingatiwa kuwa,
ndoa za siku hizi zikidumu miaka miwili Mungu mkubwa!
Mzee Mohamed Khalfan akipozi na mkewe, Bi. Habiba Shomari.
Muda mwingi vikongwe hao walikuwa
wakipelekeana midomo na kumwaga mabusu mazito. Baadhi ya watu walisema
kwa kizazi cha sasa kuna cha kujifunza kwa vikongwe hao ingawa wenyewe
walidai siri ya ndoa yao kudumu ni kuvumiliana na kuheshimiana.
tiko
tiko
Post a Comment